Pages

Tuesday, 28 October 2014

TAMBUA HAYA

Reel to Reel tape recoder iliyokuwa ikitumika zamani na redio Zanzibar,kurecord na kutunza taarifa mbalimbali.
Hizi ni kochi zilizotengenezwa kwa miti kisiwani Unguja.
Hii ni picha ya meno ya Tembo iliyopo makumbusho ya Zanzibar.Watu wengi huita pembe za Ndovu,kiuhalisia zinaitwa meno ya Ndovu au Tembo.

Hizi ni ngazi 100 zilizopo ufukweni mwa bahari ya Hindi Zanzibar,watu huzitumia kwa ajili ya mazoezi.

KUMBUKUMBU YA UTUMWA ZANZIBAR

Kumbukumbu ya utumwa wa mwafrica,hizi sura za sanamu ni za uhalisia ya baadhi ya wazanzibar.
Chumba cha mtumwa askari aliyekuwa akichunga wenzake.
Sanamu zinazoonyesha biashara ya utumwa.
Baadhi ya chumba kilichotumika kuhifadhi watumwa kabla ya kuuzwa.


Monday, 27 October 2014

TEMBEA UONEE

  Huyu ndie samaki taa  (Sting ray)
Mjue tumbili chokoraa akiwa kazini.
Sungura akila bata mjin nae ni msomi yupo chuo cha A3 Institute of Professional Studies.






Sunday, 26 October 2014

VITAMUUUU

Mishikaki ya kila aina ikiuzwa maeneo ya forodhani Unguja.
Baadhi ya viungo vinavyouzwa katika soko dogo lililopo Unguja.

TEMBELEA MAENEO YA CHUO CHA MLIMANI DSM

Hii ni sehemu mojawapo ya maeneo ya chuo yenye kuvutia.
Sehemu ya msitu mdogo uliopo chuoni.
Sehemu ya jengo la ukumbi wa chuo cha mlimani uliojengwa mfano wa sarafu iliyotumika zamani ya shilingi tano.

FURAHIA VITUKO VYA WANYAMA CHUO KIKUU CHA MLIMANI DAR - ES - SALAAM

Tumbili  wanapiga chabo dirishani katika moja ya nyumba za mlimani, kinachoendelea ndani  ni nini.
Tumbili wakibadilishana mawazo katika maeneo ya chuo.
Mama tumbili akiwa amembeba mwanae kwa mapenzi ya sio ya kawaida

YAJUE MAZINGIRA YA CHUO CHA MLIMANI

Huyu anajulikana kwa jina la nguchiro.
Hii ni sehemu ya chuo kikuu cha Dar-es Salaam
Haya ni maeneo ya chuo kikuu cha Dar-es -Salaam sehemu ya Darajani

Friday, 24 October 2014

ENZI ZA UKOLONI

Hiki ni kiti cha wapendanao kilichopo katika nyumba ya makumbusho Zanzibar.
Viatu na pete vilivyo tengenezwa kwa mbao vya mke wa mfalme  Seyyid Khalifa vipo katika makumbusho Zanzibar.


Kumbukumbu ya kitanda cha mfalme Seyyid khalifa.

Hili ni gari lililotumiwa na Austin Princes aliyekuwa balozi wa kiingereza kabla ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.



TENGENEZA KIASILI

Kochi lililo tengenezwa kwa miti na kamba za katani.
Chombo cha kujimwagia maji wakati wa kuoga kimetengenezwa kwa kifuu cha nazi na mshikio wa mti kimewekwa juu ya stuuli.
Kiti kilichotengenezwa kwa miti na ngozi ya mbuzi.
Feni iliyotengenezwa kwa majani ya makuti.


UPAMBAJI WA ASILI

Baadhi ya matangazo yaliyowekwa katika hoteli zilizoko Zanzibar.
Hili ni ua lililo oteshwa katika kichungi cha makuti.
Huu ni mtumbwi ambao umefanyika kuwa sehemu ya kuwekea mapambo.
Ua limeoteshwa katka kichungi kilichosukwa kwa kamba za katani,chini yake ni kichanja na watu hupumzika kwa chini


Thursday, 23 October 2014

WANYAMA MBUGANI

Simba dume akiwa katika hifadhi ya Ngorongoro,kwa kawaida simba dume siyo mwindaji.
Simba jike mwindaji mashuhuri.
.
Upepo mwanana anaoufurahia simba jike baada ya uchovu wa kuwinda,  katika hifadhi ya Serengeti.
Twiga wakiwa katika mbuga ya Serengeti.
Wanyama wahamiaji wakiwa katika hifadhi ya Ngorongoro,wakati wa kiangazi wanyama huwa na tabia ya kuhama kwenda nchi ya jirani Kenya kwa ajili ya kutafuta maji.

MATUNDA KWA AFYA

Ndizi aina ya malindi hupikwa,  na kuliwa kama chakula, na pia huvundikwa na kuiva huliwa kama tunda,madafu hutoa maji  kinywaji.
Mkonge wa tembo ni ndizi ambazo zinafaa kupikwa na kukaangwa.
Ndizi hupikwa kwa kuchanganya na viazi vitamu.
Matunda aina ya tikiti maji na embe dodo.


UBUNIFU WA VITU VYA ASILI

Mlango uliotengenezwa zaidi ya mika 50 iliyopita, katika mji wa mawe (stone town) kisiwani Unguja Zanzibar,umetengenezwa kwa mbao na kuwekwa urembo ambao ni silaha pia kwa ajili ya kuzuia tembo wasiweze kuvunja na kuingia ndani.Tembo walikuwa wakivamia mji huu mara kwa mara enzi ya ukoloni.
Hiki ni kifuu cha nazi kilichotengenezwa kwa ustadi wa kiasili, ni chombo kinachotumika kuwekea majivu ya sigara (Ashtray)
Dada huyu ana ushangaa mti uitwao mkadi wenye mizizi mingi ambayo hutumika kama ukili wa kutengenezea vitu,mfano mikeka na vikapu,mti huu upo katika hifadhi ya Johazi Chwaka bay Kisiwani Unguja.Ina aminika pia mizizi ya mti huu hutumika kuongeza nguvu za kiume.
Vikapu vilivyotengenezwa kwa ukili.
Sehemu ya mtumbwi inayotumika kusafirisha wavuvi wanapokuwa baharini wakivua samaki.

IJUE JOZANI CHWAKA BAY


Kima wekundu (Punju) wapo katika hifadhi ya Jozani Chwaka Bay (National Park Zanzibar) umri wao wa kuishi ni kati ya miaka 20 na 25,wana rangi ya kuvutia iliyochanganyikana nyeusi na nyekundu,kundi moja laweza kuwa na kima 15 hadi 20.
Miti ya asili iliyopo katika hifadhi zaidi ya miaka 50.
Hii ni mizizi inayojumuisha miti mitatu kwa pamoja,Ficus,Nataiensis na Mandege.
Sehemu ya daraja lililopo ndani ya hifadhi ya Jozani.


Baadhi ya miti aina ya mitondoo iliyodondoka katika hifadhi,hairuhusiwi kukatwa kuni wala kuchoma moto.