Pages

Monday, 13 October 2014

MCHAGGA NA ASILI YA MLIMA KILIMANJARO





Mlima Kilimanjaro upo kasikazini mwa Tanzania,katika mkoa wa Kilimanjaro,ni mlima mrefu kuliko yote katika Bara la Afrika,una urefu wa mita 5895 na futi 19340 kutoka usawa wa bahari.Mlima huu ni kivutio kikubwa sana kwa wageni wa ndani na nje ya nchi.



Mandhari inayozunguka mlima huu pia umezungukwa na vivutio vingi ikiwamo wanyama kadhaa katika msitu unaozunguka mlima huu wakiwemo Mbega,Nyani,Nyati, Chui,Tembo,Swala na ndege wazuri,hifadhi ya mlima ina kilometa za mraba 755,vilele vya mlima huu ni Kibo, Mawenzi na Shira,kilele cha juu kabisa ni Kibo na mtu wa kwanza kufika kileleni alikuwa ni Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu akiwaongoza wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller  mwaka 1889.

Miaka nenda rudi wachagga wenyewe hawakujua ya kwamba upo Mima Kimanjaro.Mzee Bernard Ndewingia kutoka Kirua Vunjo (KV),alielezea maana halisi ya Mlima Kilimanjaro ilitokana na pale  alipokuja missionary Redmann na kugundua mlima huu,Wachagga kwa taharuki wakasema KILIMA KYARO,ikiwa na maana kilima ni mlima,kyaro umeota.Wao walidhani ule mlima ulikuwa haupo na ndo Redmann alipougundua ndo ulikuwa umeota.Pia watu wengi hasa kutoka nje ya nchi wanauelewa potofu kuwa mlima huu upo nchi jirani ya Kenya kitu ambacho sio kweli.

Tuna haki ya kujivunia Kilimakyaro (Mlima Kilimanjaro) kwani ni kitega uchumi cha taifa letu na watanzania tuwe na desturi ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini tusisome tuu katika historia na kuhadithiwa.
Nyani akiwa katika mti akifurahia maisha.
Kanga wakiwa katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment