Dada wa kimasai aliye valia vazi la kimasai. |
Hii ni nyumba ya kimasai iliyojengwa kwa ustadi mkubwa sana na ya kupendeza,imetengenezwa kwa kutumia miti miyembamba yaan fito,majani ya migomba yale ambayo yanatokana na shina la mgomba na si matawi yake pamoja na mavi ya ng'ombe.
Ujenzi wa nyumba kwa mila na desturi ya wamasai hujengwa na wanawake,katika boma huwa kuna kuwa na nyumba zaidi ya kumi na hiyo ni familia moja.Wanawake waliopo katika boma ndio haswa hushirikiana katika ujenzi wa nyumba,Majani yanayotumika kuezeka huanzia juu ya paa hadi chini,ndani ya nyumba chini huwekwa sakafu ambayo ni mavi ya ng'ombe hutumika kusakafia,juu ya paa huwekwa kitu cha urembo kama vile kibuyu kikubwa na pengine hata fuvu la kichwa cha ng'ombe au mbuzi.
No comments:
Post a Comment