Pages

Thursday, 23 October 2014

UBUNIFU WA VITU VYA ASILI

Mlango uliotengenezwa zaidi ya mika 50 iliyopita, katika mji wa mawe (stone town) kisiwani Unguja Zanzibar,umetengenezwa kwa mbao na kuwekwa urembo ambao ni silaha pia kwa ajili ya kuzuia tembo wasiweze kuvunja na kuingia ndani.Tembo walikuwa wakivamia mji huu mara kwa mara enzi ya ukoloni.
Hiki ni kifuu cha nazi kilichotengenezwa kwa ustadi wa kiasili, ni chombo kinachotumika kuwekea majivu ya sigara (Ashtray)
Dada huyu ana ushangaa mti uitwao mkadi wenye mizizi mingi ambayo hutumika kama ukili wa kutengenezea vitu,mfano mikeka na vikapu,mti huu upo katika hifadhi ya Johazi Chwaka bay Kisiwani Unguja.Ina aminika pia mizizi ya mti huu hutumika kuongeza nguvu za kiume.
Vikapu vilivyotengenezwa kwa ukili.
Sehemu ya mtumbwi inayotumika kusafirisha wavuvi wanapokuwa baharini wakivua samaki.

No comments:

Post a Comment